<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>110</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Mapya ni mapenzi hayo,
 Asubuhi tunayo,
 Saa za giza hulindwa
 Kwa uzima kuamshwa.

[V2]
 Kila siku, Mapya pia
 Rehema, wema, na afya,
 Wokofu, na msamaha,
 Mawazo mema, furaha.

[V3]
 Tukijitahidi leo
 Na mwendo utupasao,
 Mungu atatueleza
 Yatakayompendeza.

[V4]
 Mambo yetu ya dunia
 Mungu atayang'aria,
 Matata atageuza
 Yawe kwetu ya Baraka.

[V5]
 Yaliyo madogo, haya
 Mungu tukimfanyia,
 Yatosha: tutafaidi
 Huvuta kwake zaidi.

[V6]
 Ewe Bwana, siku zote,
 Tusaidie kwa yote:
 Mwendo wetu wote vivyo,
 Uwe kama tuombavyo.</lyrics>
<title>Mapya Ni Mapenzi Hayo TZR110</title>
</song>